• HABARI MPYA

  Tuesday, March 27, 2012

  SEVILLA YAKARIBIA ULAYA

  Manu del Moral
  MABAO mawili ya Manu del Moral yalikuwa msaada mkubwa kwa Sevilla ikiifunga Granada 3-0 na kuzidi kupaa katika La Liga katika juhudi zake za kuwania kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.
  Jose Antonio Reyes alimkatia pande safi Alvaro Negredo dakika ya 39, akafunga bao la kwanza kwenye Uwanja wa Los Carmenes.
  Negredo alimtengenezea nafasi Del Moral kufunga bao dakika ya 54 katikia mechi ya wapinzani wa Andalucian derby.
  Del Moral alifunga bao lake la pili adakika nne kabla ya filimbi ya mwisho, baada ya kuuwahi mpira uliorudi na kuihakikishia Sevilla ushindi wa pili mfululizo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SEVILLA YAKARIBIA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top