• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 27, 2012

  BOBAN NI BORA KULIKO NIYONZIMA, ASEMA MAFISANGO

  Boban katika anga za heshima na wazee wa heshima zao, alivyotulia bababe kama sio wa Mawela
  KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango, anayechezea Simba SC, anaamini Haruna Moshi 'Boban' ni bora kuliko Haruna Niyonzima wa Yanga. Akizungumza na tovuti ya Simba, Mafisango alisema yeye amecheza na wachezaji wote hao wawili katika timu moja na pengine ndiye mtu pekee hapa nchini anayewajua wachezaji hao wawili kindakindaki.
  “Nimecheza na Haruna katika timu ya taifa ya Rwanda na ninacheza na Boban hapa Simba. Bila ya upendeleo wowote, Boban ni zaidi ya Niyonzima. Hii ni kwa uwezo binafsi (technic) na kiufundi (tactic),” alisema.
  Alisema ukitaka kujua tofauti ya Boban na Niyonzima angalia tofauti iliyopo kwenye nani mwenye pasi nyingi zilizosababisha magoli na yupi mwenye magoli mengi ya kufunga baina ya wachezaji hao wawili.
  “Niyonzima anajua mpira. Lakini Boban ana mambo mengi ya ziada. Pasi nyingi za Niyonzima si za hatari lakini za Boban ni za hatari kwa maana zinaweza kusababisha lolote lile. Si lazima iwe pasi ya kuzaa goli lakini pia inaweza kuwa pasi iliyosababisha pasi ya bao,” alisema.
  Alisema jina la Niyonzima limepata umaarufu kwa kuwa pengine ndiye mchezaji wa Yanga mwenye kiwango cha juu zaidi kuliko wengine, lakini la Boban halivumi sana kwa vile kuna mastaa wengi Simba.
  Simba kuna Mafisango, Kazimoto, Kaseja, Kapombe, Sunzu na Boban. Wote hawa ni wachezaji wa kiwango cha juu na wanagawana sifa. Lakini inaonekana kwa Yanga nyota ni Niyo pekee na ndiyo maana anatangazwa sana ila mimi nakuambia Boban ni zaidi yake.
  Mafisango amefunga jumla ya mabao saba kwenye Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu na ndiye mchezaji wa kiungo aliyefunga mabao mengi zaidi msimu huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BOBAN NI BORA KULIKO NIYONZIMA, ASEMA MAFISANGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top