• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 27, 2012

  MAN UNITED JUU ENGLAND, ROONEY SHUJAA

  Muuwaji Rooney akisherehekea bao
  Rooney kulia baada ya kufunga akifurahia na John Evans aliyempa pasi
  BAO pekee la Wayne Rooney dakika ya 42, limetosha kuifanya Man United ijitanue kileleni mwa Ligi Kuu ya England, ikiwazidi wapinzani wao Man City kwa pointi tatu, baada ya kuilaza Fulham 1-0 kwenye Uwanja wa Old Trafford.
  Bao hilo la 28 kwa Rooney msimu huu, linaifanya United itemize pointi 73, baada ya kucheza mechi 30 sawa na City.
  United walikuwa na bahati kwa kutopigiwa penalti dakika ya 87 wakati Carrick alipomkwatua kwenye boksi Murphy aliyetokea benchi, lakini refa Michael Oliver akwachomolea Fulham.
  Matokeo hayo yanaifanya Fulham ibaki nafasi ya 13.
  Mechi ijayo, United wataifuata Blackburn wakati Manchester City watakuwa wenyeji wa Sunderland siku mbili kabla.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED JUU ENGLAND, ROONEY SHUJAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top