• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 29, 2012

  CHICHARITO ANA USONGO SI KITOTO


  Chicharito

  MSHAMBULIAJI Javier Hernandez amepania kufanya vitu adimu katika dakika za mwishoni za msimu ili kuisaidia timu yake, Manchester United kutwaa taji la 20 la ubingwa wa Ligi Kuu England.
  Mshambuliaji huyo wa Mexico, amefunga mabao 12 tu msimu huu kwa sababu alikuwa majeruhi na alikaa nje ya Uwanja muda mrefu.
  Ingawa hakuwa kwenye kikosi cha kwanza kwa muda mrefu, mshambuliaji huyo amepata mno kufanya mambo tofauti katika mechi nane zilizobaki kuhakikisha kwamba wapinzani wao, Manchester City hawaipokonyi taji United.
  "Ni sehemu ya msimu ambayo kila mchezaji anataka awepo," alisema Hernandez, au Chicharito.
  "Tupo kwenye nafasi nzuri, kwa sababu itategemea na sisi wenyewe – kama tukishinda mechi zetu zote, tutashinda ligi "
  "Ni msimu mrefu, hivyo hizo mechi chache za mwisho zina msisimko zaidi kwa kila mtu, lakini tuna nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi tena.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, pia alizungumzia namna anavyoizoea mikikimikiki ya Ligi Kuu England katika njia za kutimiza ndoto zake za kuwa mchezaji mkubwa duniani.
  "Nataka kuwa mchezaji babu kubwa duniani, hivyo natakiwa kufanyia kazi kila jambo ili kukuza mchezo wangu: mwenendo wangu, mabao na na nguvu za mwili, kwa sababu siyo mrefu au mwenye nguvu," alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHICHARITO ANA USONGO SI KITOTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top