• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 27, 2012

  AVB ULAJI HUO INTER MILAN, RANIERI ATUPIWA VIRAGO

  AVB
  KLABU ya zamani Ulaya, Inter Milan ya Italia imetangaza kumfuta kazi kocha wake Claudio Ranieri na kocha wa Chelsea, Andres Villas-Boas anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba mwishoni mwa msimu.
  Mwalimu huyo mwenye umri wa miakia 60, amekuwa katika wakati mgumu kutokana na matokeo mabaya yaliyoindama timu hiyo kiasi cha kuwa hatarini kuikosa na michuano ya Ulaya msimu ujao, ikiwa nafasi ya nane katika Serie A hivi sasa.
  Mapema Jumatatu, rais Massimo Moratti alimpa Ranieri kura ya kujiamini, lakini klabu hiyo ya Italia ilishindwa kumvumilia kufuatia kipigo cha Jumapili cha 2-0 katika Italy Derby kutoka kwa Juventus, kikiwa ni kipigo cha nane mwaka huu kwa Inter.
  "Rais Moratti na wote katika Inter tunapenda kumshukuru Claudio Ranieri na wasaizidi wake kitaaluma na jinsi walivyowajibika katika miezi hiyo," ilisema taarifa hiyo.
  "Inter inapenda pia kutangaza kwamba, imemkabidhi timu kocha Andrea Stramaccioni,."
  Ranieri alitua San Siro Septemba mwaka jana kufuatia kufukuzwa kwa Gian Piero Gasperini na akanza vizuri, akiitoa timu nafasi ya 17 hadi kupata tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya.
  Hata hivyo, mechi tisa mfululizo bila kushinda huku timu hiyo ikiwa hatarini kukosa tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao, zinamuondoa kazini wakati tayari msimu huu wamekwishatolewa  katika Ligi ya Mabingwa baada ya kutoka sare ya jumla na Olympique Marseille ya 2-2 na wapinzani wao kusonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.
  Inaaminika kwamba Stramaccioni ataiongoza Inter hadi mwishoni mwa msimu wakati klabu hiyo itakapoajiri kocha mwingine na anayepewa nafasi kubwa ni kocha aliyefukuzwa Chelsea, Mreno  Andre Villas-Boas.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AVB ULAJI HUO INTER MILAN, RANIERI ATUPIWA VIRAGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top