• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 30, 2012

  JOHN BOCCO ANG'ATUKA STARS


  Bocco  akikosa bao la wazi kwa kumlenga kipa wa Msumbiji, Joso Raphael, kwa “kishuti mtoto” wakati wa mechi yao ya kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika 2013 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Saalaam  hivi karibuni

  MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Bocco ametangaza kujiuzulu kuchezea timu ya soka ya taifa ya Tanzania, taifa Stars kuepuka bughudha za mashabiki.ShaffihSports imemnukuu Bocco akisema kwamba amekuwa akijitolea kwa hali na mali katika timu hiyo, lakini bado jitihada zake hazithaminiwi na mashabiki.Bocco amekuwa mshambuliaji kiongozi wa Taifa Stars chini ya kocha Mdenmark, Jan Borge Poulsen lakini kutokana na kufunga mabao, amekuwa akizomewa.Lakini huyo ndiye wa mabao katika Ligi Kuu ya Tanzania na kwa miaka mitatu sasa amekuwa habanduki kwenye ya wafungaji bora katika Ligi Kuu, ingawa msimu huu anatarajiwa kutunukiwa kiatu cha dhahabu kwa mara ya kwanza baada ya kukikosakosa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JOHN BOCCO ANG'ATUKA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top