• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 31, 2012

  BABAYARO AWAPASHA TENGA NA WENZAKE WOTE, AWAITA MUMIANI WA SOKA AFRIKA


  Babayaro akizungumza Nairobi jana

  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga na viongozi wote wa kandanda Afrika wamepashwa ukweli wao na beki wa zamani wa Chelsea, Celestine Babayaro, kwamba wanaua soka barani kwa ubinafsi wao.
  Babayaro amekaririwa na tovuti ya Super Sport akisema kwamba kukosekana kwa miundombinu na uongozi bora umekuwa sababu ya kuzoretesha maendeleo ya soka Afrika.
  Babayaro alisema kwamba kulikuwa kuna vipaji vingi Afria, lakini uongozi mbovu katika soka umeua mchezo.
  “Tuna vipaji babu kubwa Afrika. Lakini hao wanaoongoza mchezo si wakweli, kwa sababu baadhi wanautumia mchezo kwa maslahi yao binafsi.
  Wengine wanatumia kwa ajili ya kujijenga kisiasa na kusahau vijana, ambao wanahangaika kutafuta maisha. Pamoja na kuboresha miundombinu katika soka, kwa kuweka mipango mizuri, tunaweza kulingana na nchi za Ulaya, kama Italia na Hispania,"alisema Babayaro.
  Babayaro ambaye yupo Nairobi pamoja na kocha wake wa zamani wa Chelsea; Ruud Gullit kama mabalozi wa Kombe la UEFA, wamelisindikiza Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya ambalo liko ziarani katika nchi za hapa, Tanzania, Mexico na China.
  Aliwapongeza timu ya taifa ya Zambia kwa kutwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika na kusema kwamba hakuna timu ndogo wala kubwa katika soka.
  Babayaro alisema kuchezea Chelsea kwa zaidi ya miaka nane chini ya makocha wane tofauti, tangu 1987 hadi 2005 yanabaki kuwa mafanikio makubwa upande wake kwenye soka.
  “Kucheza chini ya makocha wane tofauti wakiongozwa na Ranieri, Ruud Gullit, na Jose Mourinho imenisaidia kukuza upeo wangu wa soka.
  Nimestaafu kwa heshima kubwa na ninajivunia kuhusishwa na mipango ya maendeleo ya vijana niliporejea Nigeria.”
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BABAYARO AWAPASHA TENGA NA WENZAKE WOTE, AWAITA MUMIANI WA SOKA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top