• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 28, 2012

  REFA AWAPA WATANO KADI NYEKUNDU CHUMBANI

  Kocha wa Bradford
  REFA aliwapa kadi nyekundu wachezaji watano katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya mechi ya Ligi Daraja la Nne England, League Two kati ya Bradford City na Crawley Town.
  "Siwezi kuamini kilichotokea," alisema kocha wa Bradford, Phil Parkinson, ambaye awali wachezaji wake watatu walipewa kadi nyekundu jana katika mechi hiyo, ambayo walifungwa 2-1 nyumbani.
  "Sijawahi kukutana na mazingira kama haya, refa anakuja chumba cha kubadilishia nguo, anawaweka wachezaji upande mmoja na kuwapa kadi nyekundu. Hakuniruhusu kufanya chochote pale."
  Wachezaji sita wa Crawley na mmoja wa Bradford walipewa kadi za njano katika mechi hiyo, Andrew Davies wa Bradford, ambaye alipewa kadi nyekundu, sasa anajiandaa kutumikia adhabu ya kukosa mechi tano baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu mara mbili awali msimu huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REFA AWAPA WATANO KADI NYEKUNDU CHUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top