• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 27, 2012

  SUPER MARIO BALOTELLI AZAMIA PRESS YA INTER MILAN

  Balotelli
  MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Mario Balotelli leo alisababisha timbwili tena baada ya kuzamia kwenye Mkutano Maalum na Waandishi wa Habari wa klabu yake ya zamani, Inter Milan kumtambulisha kocha wao mpya,  Andrea Stramaccioni.
  Kocha huyo wa zamani wa Inter Primavera (kikosi cha pili), ambaye ameiongoza timu yake kwenye fainali ya michuano ya NextGen Series, aliteuliwa kumrithi Claudio Ranieri katika kikosi cha wakubwa cha Inter jana.
  Katika mkutano wake wa kwanza na Waandishi wa Habari kama bosi wa Nerazzurri ya wakubwa, alisumbuliwa wakati Balotelli alipovamia chumba cha mkutano.
  Mshambuliaji huyo wa City alimsalimia Stramaccioni na Wakurugenzi wa Inter waliokuwapo.
  Kocha huyo mpya aliwatekeleza waandishi kwa muda na kusalimiana na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21, kisha akarejea na kuuliza: “Swali la mwisho lilikuwa nini?”
  Kocha huyo mwenye umri wa miaka 36, mapema alielezea mikakati yake Inter inayosuasua hivi sasa, akisema anataka kurejesha mafanikio ya enzi za Jose Mourinho alipokuwa San Siro.
  Balotelli aliondoka Inter kwenda City majira ya joto 2010.
  Amekuwa akichukuliwa kama mtukutu tangu ametua England, ingawa amelipa fadhila kwa kocha wake Roberto Mancini kwa mabao yake 15 aliyofungia msimu huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SUPER MARIO BALOTELLI AZAMIA PRESS YA INTER MILAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top