• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 26, 2012

  MACHAKU AFUNGUKA BAADA YA KUFANYA MAMBO NA SETIF

  Salum Machaku katikati ya refa na kipa wa Setif
  KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Machaku Salum, amewataka wapenzi na washabiki wa klabu yake kuzidi kumwamini ili apate nafasi zaidi ya kuonyesha uwezo wake.
  Akizungumza na tovuti ya Simba, Machaku alisema anaamini kuwa ana uwezo wa kutosha wa kucheza soka isipokuwa alihitaji muda kidogo ili kuzoeana na wenzake msimu huu na sasa ndiyo ameanza kuonyesha kiwango chake.
  Machaku amecheza mfululizo katika mechi tatu zilizopita za Simba, huku akicheza kwa dakika zote tisini katika mchezo wa Kombe la CAF kati ya Simba na ES Setif na washabiki wa klabu yake wameonyesha kufurahishwa na kiwango chake.
  "Najua kwamba mwalimu (Milovan) ana imani kubwa na mimi. Ndiyo maana unaona ananipa nafasi anazonipa. Naamini hafanyi hivi kwa upendeleo bali kwa sababua ananiona mazoezini na kwenye mechi. Nitaendeleza jitihada zaidi ili nifanikiwe zaidi," alisema.
  Machaku amesajiliwa msimu huu akitokea timu ya soka ya Mtibwa kutoka Turiani Morogoro na miezi michache iliyopita alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa hawapati sapoti ya kutosha kutoka kwa washabiki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MACHAKU AFUNGUKA BAADA YA KUFANYA MAMBO NA SETIF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top