• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 28, 2012

  MASTAA WATANO WALIOPATA WATOTO BAADA YA MIAKA 40

  Salma Hayek alisubiri hadi alipotimiza miaka 40 kuwa mke na mama. Machi mwaka 2007, mwigizaji huyo mzaliwa huyo wa Mexico alitangaza ana uja uzito na amechumbiwa na bilionea wa Kifaransa, Francois-Henri Pinault. Septemba, mwaka huo, mtoto wa kike, Valentina Paloma alizaliwa. Wazazi hao walitengana miezi 10 baadaye – lakini baadaye walirudiana na kuona katika Valentine’s Day ya mwaka 2009.
  Mariska Hargitay alikuwa ana umri wa miaka 41wakati anajifungua mtoto wake wa kiume, August, Juni mwaka 2006. Mwigizaji huyo wa “Law & Order: SVU” , akiwa na mumewe, Peter Hermann, Aprili 2001, walipata mtoto wa kike Amaya na miezi sita baadaye, wa kiume Andrew Nicolas.
  KAMA hukuwa karibu na Radio, TV, Internet, magazeti au majarida mwaka jana inaweza kuwa ulipitwa habari kwamba Mariah Carey akiwa ana umri wa miaka 41, Aprili mwaka jana alijifungua pacha kwa mumewe Nick Cannon – mtoto wa kiume walimpa jina Moroccan na wa kike Monroe. Amefikisha miaka 42, Machi 27, mwaka huu.
  Baada ya ndoa zake mbili ‘kufa’ – moja mcheza kikapu nyota David Justice na nyingine na mwanamuziki David Justice – mwigizaji Halle Berry alipata penzi jipya, mwishoni mwa mwaka 2005 na mwanamitindo Gabriel Aubry na kuzaa naye mtoto wa kike, Nahla, Machi 2008, wakati huo Berry akiwa ana miaka 41. Inauma wawili hao waliachana miaka miwili baadaye. Licha ya kusema hataolewa tena, Berry alitangaza uchumba wake na mwigizaji wa Kifaransa, Olivier Martinez wiki chache zilizopita. Je, akiwa ana umri wa miaka 45 tutarajie watoto zaidi kutoka kwake?
  Baada ya kuishi ‘kisista duu’ sana, Helen Hunt alijifungua mtoto wake wa kwanza, binti Makena Lei, Mei mwaka 2004, mwezi mmoja kabla ya mwigizaji huyo wa picha la “Mad About You” kutimiza miaka 41. Hunt, amekuwa kwenye mahusiano na Mtayarishaji wa vipindi cya Televisheni, Matthew Carnahan kwa zaidi ya muongo mmoja.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MASTAA WATANO WALIOPATA WATOTO BAADA YA MIAKA 40 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top