• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 29, 2012

  CHISORA AKATA RUFAA ARUDISHIWE LESENI YAKE


  Watoto wa kiume wanawekeana mkwara, Haye kulia na Chisora kushoto
  Haye anapambana ma msitu wa watu kumfuata Chisora
  Chisora anamchimba mkwara Haye sambamba na kumsukumia konde
  Haye anajibu konde kwa Chisora

  MWEZI mmoja baada ya kugombana na David Haye katika mkutano na Waandishi wa habari, Dereck Chisora leo amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa kumpokonya leseni yake ya ndondi ya Uingereza.Mbabe huyo wa uzito wa juu mwenye umri wa miaka 28, alipokonywa leseni yake kufuatia kikao cha saa nne cha bodi ya Ngumi Uingereza (BBBC) kilichofanyika Machi 14, mwaka huu.“Kilichomo ndani ya rufaa yetu ni kwamba hatujaridhishwa na suala zima,” alisema Frank Warren, peomota wa Chisora. “Dereck Chisora atasimama upande wake kisha tutaona nini kitatokea.”Baada ya kupigwa na Vitali Klitschko mjini Munich, Februari 19, Chisora aliingia kwenye ugomvi na bingwa wa zamani wa WBA, Haye katika Mkutano na Waandishi wa Habari.
  Kabla ya pambano lake hilo, Chisora alimchapa kibao kaka wa mpinzani wake, Wladimir Klitschko kwenye zoezi la upimaji uzito na badaaye akiwa ulingoni, akamwagia maji nje ya ulingo usoni wakati anamuangalia ndugu yake.Chisora alikuwa anatafutwa na Polisi wa Ujerumani baada ya kupigana na Haye.BBBC iliamua kwamba Chisora “hastahili kumiliki leseni ya.” Lakini Warren anakana uamuzi huo.Kama Chisora atarejeshewa leseni yake, Warren alisema anatarajia watapanda ulingoni tena na Haye.“Naona pambano litakuja. Ni eneo mwafaka kwao kumaliza tofauti zao,” alisema Warren.Pamoja na hayo, Haye bado anasakwa na Polisi wa Ujerumani na pia atatakiwa kujibu tuhuma kadhaa iwapo ataamua kurejea ulingoni baada ya kutangaza kustaafu.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHISORA AKATA RUFAA ARUDISHIWE LESENI YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top