• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 28, 2012

  TFF KIBOKO, WAWAPA CHEKI MAGUMASHI WANAJESHI

  UONGOZI wa klabu ya Ruvu Shooting umesema unasikitishwa na kitendo cha Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kuwapa hundi 'feki' na kukaa kimya kuwalipa Sh 5 milioni wanazodai tangu mwaka 2010.
  Akizungumza kwa simu kutoka Ruvu mkoani Pwani jana, meneja wa Ruvu Shooting, Narcis Ndunguru alisema kuwa fedha wanazodai ni zile zinazotolewa na wadhamini kwa klabu zote zinazoshiriki  Ligi Kuu kwaajili ya kugharimia usafiri na malazi.
  "Ndugu hapa tunapoongea tunaidai TFF sh5,447,500 za usafiri na malazi tangu mwaka 2010 wamekuwa wakitupiga danadaga tu.
  "Tunashangaa kwanini hawatulipi wakati ni haki yetu, lakini kama wadhamini wanatoa hela zinaenda wapi?.,"alisema Ndunguru.
  Alifafanua zaidi kwa kusema kuwa awali Novemba 3, 2011,TFF iliikabidhi klabu hiyo hundi yenye namba 981944, lakini chakusikitisha ni kwamba walipoipeleka benki waliambiwa ni feki na ndipo walichukua jukumu la kuirudisha ingawa alidai tangu wakati  shirikisho hilo halijawalipwa zaidi ya kuwazungushwa.
  "Hawajamaa wametuzungusha sana, kila siku njoo kesho njoo kesho, kifupi ni kwamba awaliTFF ilipotupa hundi hewa, hii ilibainika  baada ya kuipeleka benki Novemba 18, 2010, kinachoshangaza inakuaje tupewe hundi feki? na kama akaunti yao ilikuwa haina hela kwanini waliitoa,ili ni kosa kubwa,"alisema Ndunguru.
  Aliongeza kuwa Agosti 27 mwaka jana waliiandikia barua TFF kuwakumbusha juu ya deni lao ambapo waliahidiwa kulipwa  ingawa alidai ahadi hiyo pia haijatekelezeka mpaka sasa.
  "Baada ya ukimya wao tuliwandikia barua lakini waendeleleza sera ile ile ya tutawalipa sasa mpaka lini wakati na sisi tunamipango yetu?.,"alihoji Ndunguru
  Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alipotafutwa ili aweze kujibu malalamiko hayo ya Ruvu Shooting alisema wenye nafasi nzuri ya kulizungumzia ni kamati ya ligi ingawa jitihada za kumsaka mwenyekiti wa kamati hiyo Wallace Karia ili atoe ufafanuzi wa suala hilo ziligonga mwamba huku simu yake ya mkononi ikiita bila majibu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF KIBOKO, WAWAPA CHEKI MAGUMASHI WANAJESHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top