• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 31, 2012

  GYAN MFALME WA MABAO UMANGANI


  Gyan

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana, Asamoah Gyan sasa ni mfungaji bora katika Ligi Kuu ya Falme za Kiarabu (UAE), baada ya kufunga mabao mawili jana timu yake, Al Ain ikiifunga Baniyas 3-0 na kutimiza mabao 15.
  Gyan alipewa kadi ya njano kwenye mechi hiyo kwa kuzinguana na Mohammed Jaber wa Baniyas ambaye pia alipewa kadi hiyo kwa sababu hiyo.
  “Ni sehemu ya mchezo unaweza kuzinguliwa na wakati fulani watu wanakuwa wamechanganyikiwa, lakini tuliombana radhi baadaye na sasa ni poa.” Alisema Gyan alipohojiwa baada ya mechi kwenye Uwanja wa Tahnoon Bin Mohammed.
  Mchezaji huyo anayecheza kwa  mkopo kutoka Sunderland anaikimbiza Al Ain katika taji la 10. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GYAN MFALME WA MABAO UMANGANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top