• HABARI MPYA

    Friday, March 30, 2012

    OMAN YANUSA OLIMPIKI, SENEGAL KAZI WANAYO


    Senegal na Morocco

    SIMBA wa Teranga, Senegal watamenyana na Oman katika mechi maalum ya kuwania tiketi ya kucheza Olimpiki mwaka huu, London, mchezo utakaofanyika Aprili 23 mjini Coventry.
    Mechi hiyo itaamua timu ya mwisho yab kukamilisha idadi ya timu 16 za kucheza Olimpiki inayotarajiwa kuanza Julai 26 hadi Agosti 11, mwaka huu.
    Simba wa Teranga wamepata nafasi hiyo baada ya kushika nafasi ya nne katika michuano ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 23 iliyofanyika Morocco Desemba mwaka jana.
    Oman inayofundishwa na Mfaransa, Paul Le Guen walipata nafasi hiyo baada ya kuifunga Uzbekistan 2-0 Alhamisi katika mechi ya mwisho ya kuwania kufuzu kucheza fainali hizo kwa bara la Asia.
    Gabon, Morocco Misri ni wawakilishi wengine wa Afrika kwenye Olimpiki ya mwaka huu.
    Timu nyingine zilizofuzu ni mbali na wenyeji Uingereza, ni Korea Kusini, Japan, Falme za Kiarabu kwa Asia (AFC); Brazil na Uruguay kwa Amerika Kusini (CONMEBOL); Uswisi, Hispania na Belarus kwa Ulaya (UEFA) na New Zealand (OCEANIA).
    Wawakilishi wengine wawili watoka Amerika Kaskazini, CONCACAF ambao michuano yao inatarajiwa kumalizika Jumatatu ijayo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OMAN YANUSA OLIMPIKI, SENEGAL KAZI WANAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top