• HABARI MPYA

  Jumanne, Machi 27, 2012

  MESSI SAWA, LAKINI MSIMSAHAU IBRA


  Ibra alipomkuwa Barca
  WAKATI mashabiki wengi bongo wakisubiri kwa hamu kumshuhudia Lionel Messi atafanya maajabu gani kesho Barca ikimenyana na AC Milan, upande wa pili itakuwa nafasi nzuri kwa Zlatan Ibrahimovic kuthibitisha kitu fulani usiku huo katika mechi hiyo ya kwanza ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa.
  Ikumbukwe Ibrahimovic alikuwa ana msimu mgumu sana alipokuwa Barcelona kabla ya kutimkia Milan.
  Lakini Jumamosi, alifunga bao lake la 29 msimu huu, Milan ikishinda 2-1 dhidi ya Roma.
  Makamu wa rais wa Milan, Adriano Galliani alisema: “Tumekutana na mabingwa wengi, huyu anaonekana kubwa bora zaidi.”
  Katika Ligi ya Mabingwa, Ibrahimovic amefunga mabao matano kwenye mechi sita wakati Messi, pia amefunga idadi hiyo hiyo, ingawa yeye yote alifunga kwenye mechi moja tu dhidi ya Bayer Leverkusen Barca ikishinda 7-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI SAWA, LAKINI MSIMSAHAU IBRA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top