• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 28, 2012

  REAL, CHELSEA ZANUSA NUSU FAINALI ULAYA

  Fernando Torres (katikati) wa Chelsea na Jardel (kulia) wa Benfica usiku huu kwenye Uwanja Estadio da Luz, Lisbon.
  KLABU za Chelsea na Real Madrid usiku huu zimeshinda mechi zao za kwanza za Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutinga Nusu Fainali.
  Salomon Kalou aliunganisha krosi ya Fernando Torres dakika ya 75, kuipatia Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya Benfica mjini Lisbon, Ureno, huo ukiwa ushindi wa kwanza ugenini kwa The Blues kwenye mashindano hayo msimu huu.
  Nchini Cyprus, Karim Benzema alifunga bao la kichwa cha mkizi dakika ya 74, Kaka akapiga la pili dakika ya 82 na  Benzema akafunga tena dakika ya 89 kuwapa mabingwa hao mara tisa, Madrid ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji APOEL Nicosia.
  Mechi za marudiano zitachezwa Aprili 4, mwaka huu.
            Beki Mreno wa Real Madrid, Pepe akiwarukia wenzake baada ya Mbazil, kiungo Kaka kufunga kwenye Uwanja wa GSP, mjini Nicosia usiku huu.
  Jumatano katika mfululizo wa Robo fainali za michuano hiyo, mabingwa watetezi Barcelona watamenyana na AC Milan na Marseille watakuwa wenyeji wa Bayern Munich.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL, CHELSEA ZANUSA NUSU FAINALI ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top