• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 30, 2012

  ANCLE THOM AWAPA SIMBA SIRI ZA MAANGAMIZI

  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Thomas 'Ancle Thom' Kipese amewathazalisha wachezaji wa klabu hiyo kutokubali kucheza kwa kujihami katika mechi yao ya marudiano dhidi ES Setif ya Algeria ya kuwania Kombe la Shirikisho Afrika kama wanataka kusonga mbele.
  Akizungumza na gazeti hili jana, Kipese alisema kama kuna kosa Simba watalifanya basi ni kukaa nyuma na kucheza kwa kujihami kwa lengo la kulinda mabao yao 2-0.
  "Bahati nzuri mwaka 1993 wakati nilipokuwa nikiitumika Simba tuliwahi kucheza na timu moja kutoka Algeria na kufanikiwa kuitupa nje ya mashindano kama haya hivyo nawajua vilivyo waarabu hao.
  "Wanapokuwa ugenini hujitahidi kupata sare, lakini wapokuwa nyumba hubadilika ile mbaya hivyo wito wangu kwa wachezaji wa Simba ni kutokubali kucheza kwa kujihami wanachopaswa kwenda kufanya huko ni kucheza kwa kushambulia kama walivyocheza hapa nyumbani," alisema Kipese.
  Alisema hali hiyo itawasaidia kukabiliana na kasi ya waarabu hao ambao alidai kuwa wataingia uwanjani kwa lengo moja tu la kushambulia na kusawazisha mabao yale walipigwa hapa nchini na kupata mengine ili waweze kusonga mbele.
  Winga huyo wa zamani wa Taifa Stars, aliwataka Emmanuel Okwi, Haruna Moshi 'Bobani' Salum Machaku, Felix Sunzu pamoja na Mafisango kujituma zaidi ya walivyocheza kwenye mechi yao ya kwanza iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa wiki iliyopita ili kuhakikisha wanaitupa nje ya mashindano ES Setif.

  Kipese alikuwamo kwenye kikosi cha Simba SC mwaka 1993, kilichoitoa Al Harrach ya Algeria katika Robo Fainali ya Kombe la CAF na kufanikiwa kufika hadi fainali ilipofungwa na Stella Abidjan ya Ivory Coast. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ANCLE THOM AWAPA SIMBA SIRI ZA MAANGAMIZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top