• HABARI MPYA

  Alhamisi, Machi 29, 2012

  WLADIMIR ULINGONI JULAI 7


  Wladimir

  BINGWA wa ngumi za uzito wa juu, Wladimir Klitschko Julai 7, mwaka huu atapanda ulijngoni kusaka ushindi wa pambano la 16 mfululizo na Knockout (KO) ya 12 katika kipindi hicho, katika pambano la marudiano na Tony Thompson nchini Uswisi, amesema Mshauri wa Klitschko, Shelly Finkel jana.
  Pambano hili linakuja miaka minne tangu bondia hyuyo mwenye urefu wa futi 6.7, Klitschko mwenye rekodi ya 57-3, KO 50 amshinde kwa KO raundi ya 11 mpinzani wake huyo mwenye urefu wa 6.5, Thompson mwenye rekodi ya (36-2, Ko 24).
  Thompson alitangaza pambano la marudiano na mbabe huyo wa dunia katika ukurasa wake wa Facebook.
  Klitschko, aliyetimiza miaka 36, Machi 25, atapanda ulingoni akiwa na kumbukumbu ya kushinda kwa KO raundi ya nne dhidi ya bingwa wa zamani wa uzito wa Cruiser, Jean Marc Mormeck Machi 3, mwaka huu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WLADIMIR ULINGONI JULAI 7 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top