• HABARI MPYA

  Jumatano, Machi 28, 2012

  SPURS NA CHELSEA, EVERTON NA LIVERPOOL NUSU FAINALI KOMBE LA FA

  Mchezaji wa Tottenham, Kyle Walker akishangilia usiku huu.
  KLABU ya Tottenham imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bolton katika Robo Fainali ya Kombe la FA usiku huu, siku 10 baada ya kuvunjika kwa mechi ya kwanza kufuatia kuzimia kwa kiungo wa wapinzani wao uwanjani Fabrice Muamba kwa matatizo ya moyo.
  Mabao ya Ryan Nelsen, Gareth Bale na Louis Saha katika dakika 16 za mwisho dnio yaliyoipa Spurs tiketi ya Nusu fainali, ambako watakutana na wapinzani wao katika jiji la London, Chelsea kwenye Uwanja wa Wembley Aprili 15.
  Ilikuwa ni mechi ya kukumbusha majonzi kwa timu zote kwenye Uwanja wa White Hart Lane, kukumbukia jinsi Muamba alivyoanguka na mapigo ya moyo kusimama akiwa peke yake deakika ya 78.
  Alipelekwa hospitali na sasa anaendelea vizuri.
  Everton iliichapa Sunderland 2-0 katika marudio ya Robo Fainali nyingine na kutinga Nusu Fainali, ambako watakutana na wapinzani wao, Liverpool Uwanja wa Wembley, Aprili 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SPURS NA CHELSEA, EVERTON NA LIVERPOOL NUSU FAINALI KOMBE LA FA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top