• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 26, 2012

  OWEN TUMAINI JIPYA LA UBINGWA MAN UNITED

  
  Owen
  MSHAMBULIAJI Michael Owen aliyepona anaweza kutoa mchango mkubwa kwa Manchester United kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England, hiyo ni kwa mujibu wa kocha Sir Alex Ferguson.
  Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, anarejea uwanjani baada ya miezi mitano ya kuwa nje kwa majeruhi.
  United inaweza kupaa kileleni mwa Ligi Kuu kwa wastani wa pointi tatu zaidi kama itaifunga Fulham usiku wa leo na pamoja na kwamba Owen hajawa tayari kabisa, lakini Ferguson anaamini anaweza kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha United  kwenye mechi saba zilizobaki.
  "Kama unafikiria mchezaji wa kukufungia mabao muhimu, yupo yeyote zaidi ya Michael Owen?" alihoji Ferguson.
  Ferguson alisema Owen ilikuwa arudi mapema uwanjani, lakini akaumia tena mazoezini.
  "Alirejea mazozini wiki kadhaa zilizopita na kisha baada ya awamu moja wa mazoezi, akawa anafanyishwa mazoezi ya nguvu na mtaalamu wetu wa timu, akazidisha," alisema Ferguson.
  "Hivyo ilimzuia kwa siku chache, lakini ataungana nasi wiki hii."
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: OWEN TUMAINI JIPYA LA UBINGWA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top