• HABARI MPYA

  Jumamosi, Machi 31, 2012

  NIZAR KHALFAN ATEMWA PHILADELPHIA UNION MIEZI MITATU TANGU ASAJILIWE

  Nizar akishangilia moja ya mabao yake Vancouver

  Nizar mazoezini na Philadelhphia Union

  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Nizar Khalfan ametemwa na klabu ya Philadelphia Union ya Ligi Kuu ya Marekani na sasa hana timu.Habari za uhakika kutoka Marekani, ambazo bongostaz imezipata zimesema kwamba, Nizar ambaye wiki iliyopita alionekana Dar es Salaam, alitemwa na klabu hiyo miezi mitatu tu tangu achukuliwe baada ya kufuzu majaribio.Nizar alikwenda kufanya majaribio Union, baada ya kutemwa na Vancouver, Novemba 23, mwaka jana.Nizar aliyezaliwa Juni 21, mwaka 1988 mjini Mtwara, alijiunga na Vancouver Whitecaps FC ya Canada Agosti 22, mwaka 2009 akitokea Moro United ya Ligi Kuu ya Bara na akacheza mechi tisa msimu wa kwanza wa 2009 na kuongezewa mkataba wa kuichezea timu hiyo msimu uliofuata wa 2010.Alifunga bao lake la kwanza Whitecaps Juni 12, mwaka 2010 katika mechi dhidi ya Austin Aztex na haikushangaza Februari 9, mwaka jana aliposaini mkataba mpya wa mwaka mmoja baada ya timu hiyo kupanda Ligi Kuu ya Marekani, maarufu kama Major League Soccer.Hata hivyo, baada ya msimu huo timu yake ikirejea Daraja la kwanza, Niazar akatemwa na kwenda Philadelphia Union, ambako miezi mitatu baadaye ametemwa nako.Juhudi za kumpata Nizar kuzungumzia mustakabali wake zinaendelea.Kabla ya Moro United, Nizar aliyeibukia kwenye timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys mwaka 2004, alichezea
  Mtibwa Sugar FC, na baadaye akanunuliwa na Al Tadamon ya Ligi Kuu ya Kuwait msimu wa 2007-2008.Januari 2008 aliondoka Al Tadamon na kusaini mkataba na Tadamon Sour ya Lebanon, ambako alipomaliza mkataba wake akarejea Tanzania kuchezea Moro United.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NIZAR KHALFAN ATEMWA PHILADELPHIA UNION MIEZI MITATU TANGU ASAJILIWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top