• HABARI MPYA

  Ijumaa, Machi 30, 2012

  REAL ITAVUNA NINI KESHO?


  Ronaldo

  OSASUNA inaweza kumkosa Marc Bertran katika mechi na Real Madrid leo tangu matatizo yake kwenye mechi iliyopita wakishinda Levante Jumapili waliyoshinda 2-0.
  Kike Sola na Masoud Shojaei wote wapo nje kwa sababu ni majeruhi, lakini Javad Nekounam anarudi tena baada ya kumaliza adhabu yake ya mechi moja.
  Real Madrid itamkosa Jose Callejon anayeumwa kifundo cha mguu, Ricardo Carvalho (thigh) na Lassana Diarra (nyama za paja), lakini winga Angel Di Maria, ambaye amekuwa nje ya Uwanja tangu Februari kwa maumivu, anatarajiwa kurejea.
  Mesut Ozil amemaliza adhabu sambamba na kocha wake Jose Mourinho, ambaye aliikosa mechi ya ushindi wa 5-1 dhidi ya Real Sociedad baada ya kutolewa nje kwenye mechi ya sare ya 1-1 na Villarreal.
  Raphael Varane anatarajiwa kuendelea kucheza beki ya kati kutokana na kutokuwepo kwa Pepe, ambaye atakuw aanamalizia mechi yake ya pili ya adhabu.

  Vikosi;
  OSASUNA: Fernandez, Raitala, Roversio, Flano, Damia, Punal, Nekounam, Cejudo, Garcia, Lamah na
  Nino.
  REAL MADRID: Casillas, Arbeloa, Varane, Ramos, Marcelo, Khedira, Alonso, Ozil, Kaka, Ronaldo, Benzema,

  JE WAJUA?
  Osasuna wanaoshika nafasi ya sita, hawajafungwa mechi sita katika La Liga (imeshinda tat, imetoa sare tatu).
  The Pamplona wamefungwa mechi mbili tu nyumbani msimu huu – dhidi ya Racing Santander na Atletico Madrid.
  Osasuna, kwa pamoja na Racing, zimetoa sare nyingi zaidi La Liga msimu huu (13).
  Real Madrid imefungwa mechi mbili kati ya ilizokwenda Osasuna.
  Ushindi wa mwisho kwa Reyno de Navarra ulikuwa ni Mei 2008.
  Cristiano Ronaldo alifunga mawili katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Real Sociedad na kuweka rekodi ya mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 100 haraka zaidi katika historia La Liga (101 ndani ya mechi 92).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: REAL ITAVUNA NINI KESHO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top