• HABARI MPYA

    Monday, March 26, 2012

    MTEMI RAMADHAN APEWA UKATIBU MKUU TFF

    Mtemi Ramadhan kulia, akiwa na makamu wa pili wa Rais wa TFF, Nassib Ramadhan kushoto
    MWENYEKITI wa Kamati ya Ligi Kuu, Wallace Karia ameshauri Mtemi Ramadhani ndiye awe anateuliwa kukaimu nafasi ya Ukatibu Mkuu, inapotokea mhusika hayupo na si Sunday Kayuni. Akizungumza na bongostaz mchana huu, Karia alisema kwamba inavyoonekana ni kama Sadi Kawemba na Kayuni wanaelemewa na majukumu ndio maaana wanafanya ‘branda’ kibao.
    Karia alisema hayo, kufuatia akina Kayuni kushindwa kuwasilisha kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, ripoti ya hatua zilizochukuliwa na Kamati ya Ligi Kuu dhidi ya wachezaji watano wa Yanga.
    “Kwanza ilikubaliwa aajairiwe Desk Officer wa Ligi Kuu, nashangaa hadi leo kimya, Said na Kayuni inaonekana wanaelemewa, kwanza mimi nashauri ni bora kama Mtemi anakuwa yuko vizuri, ndiye akaimu Ukatibu Mkuu badala ya Kayuni.
    Kwa sasa Kayuni anafanya kazi za Katibu Mkuu wakati mwenye nafasi yake, Angetile Osiah ni mgonjwa.
    Jana Kamati ya Nidhamu ya TFF  iliwaachia huru wachezji watano wa Yanga waliokuwa wamefungiwa kucheza soka vipindi tofauti na Kamati ya Ligi Kuu.
    Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kamanda Mstaafu wa Polisi Kanda Maalum, Dar es Salaam, Afred Tibaigana alisema kwa mujibu wa taratibu za TFF, Kamati ya ligi haina mamlaka ya kumfungia mchezaji yoyote wala kutoa adhabu kwa mchezaji yeyote, ispokuwa Kamati ya Nidhamu ndo yenye mamlaka hayo.
    Tibaigana alisema kamati ya nidhamu ndo yenye wajibu wa kuwawajibisha wachezaji na viongozi wanaopatikana na hatia katika mpira wa miguu, hivyo maamuzi yaliyofanywa na kamati ya ligi sio halali, hivyo kama bado wanataka kuwashitaki tena wachezaji hao inabid wapeleke malalamiko yao upya kwa kamati ya Nidhamu.
    Awali kamati ya ligi ya mashindano iliyokutana tarehe 12.03.2012 chini ya mwenyekiti wake Godfrey Nyange Kaburu ilitoa adhabu kwa wachezaji watano (5) wa yanga kutokana na kile walichokiita utovu wa nidhamu kwa wachezaji wa yanga katika mchezo dhidi ya Azam fc, mchezo uliochezwa machi 10 mwaka huu.
    Kamati hiyo ya ligi ilitoa adhabu ya kumfungia mchezaji Stephano Mwasika mwaka mmoja kutocheza mpira na faini ya tsh milioni moja.
    Jeryson Tegete alifungiwa kutocheza ligi kuu kwa miezi sita (6) na faini ya sh.500,000.
    Nadir Haroub Cannavaro alifungiwa kutocheza ligi kuu kwa mechi sita (6) na faini ya sh.500,000.
    Nurdin Bakari alifungiwa kutocheza mechi tatu (3 )za ligi kuu na faini ya sh.500,000.
    Omega Seme alifungiwa kutocheza mechi tatu (3) za ligi kuu na faini ya sh.500,000.
    Kutokana na maamuzi ya kamati ya nidhamu - TFF wachezaji hawa watano (5) waliokuwa wamefungiwa kwa sasa wapo huru na wanaruhusiwa kucheza michezo inayofuata katika ligi kuu mpaka hapo TFF itakapopeleka malalamiko mapya juu ya wachezaji hao kwa kamati ya nidhamu.
    Klabu ya Yanga itawatumia wachezaji wake hao katika mchezo dhidi ya timu ya Coastal Union ya tanga jumamosi ijayo katika mchezo wa ligi kuu utakaofanyika jijini tanga machi 31-2012.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MTEMI RAMADHAN APEWA UKATIBU MKUU TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top