• HABARI MPYA

  Jumatatu, Machi 26, 2012

  ILIKUWA WIKIENDI MBAYA KWA MAPRO WA KENYA MAZEE


  Oboya peke yake alishangilia ushindi Slovakia
  WANASOKA wa Kenya wanaocheza nje, hawakuwa na wikiendi nzuri kwa Victor Wanyama kupata kadi nyekundu ya kwanza tangu ajiunge na Celtic katika Ligi Kuu ya Scotland, wakati Auxerre imeangukia kwenye shimo.
  Bongostaz imepitiapitia matokeo ya klabu za Wakenya juu na inakushushia kama ifuatavyo.

  Scotland:
  Celtic ilipigwa 3-2 na wapinzani wao wa jadi, Rangers sambamba na kupoteza wachezaji watatu kwa kadi nyekundu katika mechi kali na ya kibabe.
  Victor Wanyama alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na kuiacha Celtic na wachezaji tisa.

  Ufaransa:
  Timu ya Dennis Oliech, Auxerre imebaki kwenye hatari ya kushuka daraja baada ya kufungwa 1-0 na Toulouse, lakini mshambuliaji huyo wa Harambee Stars aliikosa mechi hiyo kwa sababu alikuwa anatumikia adhabu ya kadi tano za njano.
  Auxerre inashika mkia kwenye Ligi Kuu Ufaransa, ingawa Oliech amefunga mabao tisa msimu huu.

  Italia:
  Timu ya Macdonald Mariga, Parma ilitoka 2-2 na Cesena, ingawa Mariga hakucheza kwa sababu alikuwa majeruhi baada ya kuumia kwenye mechi na AC Milan wiki iliyopita.

  Slovakia:
  Mshambuliaji Patrick Oboya amekuwa kwenye kiwango kizuri na kuiwezesha timu yake, Rozoomerok kushinda 5-2 dhidi ya Zlate katika mechi tamu, ambayo Oboya alicheza kwa dakika 75.

  DRC:
  Kiungo mkongwe wa Kenya, Titus Mulama naye alikuwa kwenye majonzi baada ya timu yake, St. Eloi Lupopo kufungwa 4-2 na Black Leopards mjini Lumbumbashi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ILIKUWA WIKIENDI MBAYA KWA MAPRO WA KENYA MAZEE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top