VIUNGO wa Super Eagles, Kalu Uche na Ahmed Musa wote
walikuwa kivutio wakizichezea klabu zao Ulaya jana usiku.
Uche alicheza dakika zote 90 wakati RCD Espanyol ikishinda 3-1
dhidi ya Racing Santander kwenye Uwanja wa Cornella El Pratt.
Mnigeria huyo hakufunga bao, lakini alipiga mzigo wa uhakika na kutoa pasi za mabao akimburuza beki wa Racing na Joan Verdu, Phillipe Coutinho na Hector Moreno wakafunga mabao, hivyo kuisaidia timu yake kupanda hadi nafasi ya sita katika msimamo wa La Liga.
Uche ambaye anataka kuipeleka timu yake Europa League msimu ujao, amefunga mabao manne tangu atue timu hiyo Januari akitokea Neuchatel Xamax ya Uswisi.
Kwa upande wake, Musa, alicheza dakika 63 wakati klabu yake, CSKA Moscow ikiifunga Spartak Moscow mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Luzhniki.
Kinda huyo wa miaka 19, kwa mara ya kwanza alicheza dakika 63 kabla ya kupumzishwa na kocha wa CSKA, Leonid Slutsky akimpisha nyota wa Sierra Leone, Sekou Oliseh.
Musa amecheza mechi tano CSKA Moscow, mbili za Ligti ya Mabingwa na tatu za Ligi Kuu ya Urusi tangu atue timu hiyo Januari, akitokea VVV Venlo ya Uholanzi kwa dau la Euro Milioni 5.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Kano Pillars alifunga bao moja tu dhidi ya Zenith St Petersburg, Machi 3.

.png)
0 comments:
Post a Comment