• HABARI MPYA

  Wednesday, January 09, 2019

  SIMBA SC YAENDELEZA UMWAMBA WAKE KOMBE LA MAPINDUZI ZANZIBAR

  Na Mwandishi Wetu,  DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imekamilisha mechi zake za Kundi A kwa ushindi mfululizo baada ya kuilaza Mlandege 1-0 katika michuano ya Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi tisa baada ya kucheza mechi tatu na kuendelea kuongoza Kundi A.
  Bao pekee la Simba SC katika mchezo huo lilifungwa na kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima dakika ya 21  kwa penalti iliyotolewa na refa Rashid Farhan baada ya beki Asante Kwasi wa Simba SC kudondoshwa kwenye ndani boksi.

  Kikosi cha Mlandenge kilikuwa; Isihaka Hakim, Said Mussa, Edwin Charles, Abubakar Ali, Ali Hamduu/ Fini Salum dk33, Gerson Gerard, Ibrahim Ali, Abubakar Ame, Mohammed Abdallah, Yahya Haji/ Said Khamis dk 47 na Omary Makame/Anderson Charles dk72.
  Simba SC; Deogratias Munish ‘Dida’, Asante Kwasi, Nicholas Gyan/ Zana Coulibaly dk46, Yussuf Mlipili, Juuko Murshid/Paul Bukaka dk46, Jonas Mkude/ Said Ndemla dk45, Muzamil Yassin, Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga/Abdul Selemani dk 63, Adam Salamba na Rashid Juma/ Shiza Kichuya dk78.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAENDELEZA UMWAMBA WAKE KOMBE LA MAPINDUZI ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top