• HABARI MPYA

  Sunday, January 13, 2019

  MAN UNITED YAIPIGA SPURS 1-0 NA KUFIKISHA POINTI ZA ARSENAL

  Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao pekee dakika ya 44 akimalizia pasi ya kiungo Paul Pogba katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur leo Uwanja wa Wembley kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England.
  Ushindi huo unaifanya Manchester United ifikishe pointi 41 sawa na Arsenal baada ya wote kucheza mechi 22, ingawa inabaki nafasi ya sita nyuma ya Washika Bunduki hao wa London kwa kuzidiwa mabao mawili tu.
  Spurs inabaki na pointi zake 48 baada ya kucheza mechi 22, ikiendelea kukamata nafasi ya tatu nyuma ya Manchester City yenye pointi 50 za mechi 21 na vinara Liverpool pointi 57 mechi 22 na mbele ya Chelsea yenye pointi 47 za mechi 22 pia 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAIPIGA SPURS 1-0 NA KUFIKISHA POINTI ZA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top