• HABARI MPYA

    Monday, January 07, 2019

    KMC YAIPIGA JKT UHURU, RUVU SHOOTING YAICHAPA NDANDA NANGWANDA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) imefanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
    Ushindi huo umetokana na bao pekee na la kujifunga la Ramadhani Madenge dakika ya 40 na sasa KMC inayofundishwa na Mrundi, Etienne Ndayiragijje inafikisha pointi 28 baada ya kucheza mechi 20 na kupanda hadi nafasi ya tano kutoka ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
    JKT Tanzania inayofundishwa na Bakari Shime inabaki na pointi zake 21 ikifikisha mechi 19 za kucheza na kuendelea kukamata nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
      
    Mechi nyingine ya Ligi Kuu, leo Ruvu Shooting imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ndanda FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, bao pekee la mshambuliaji wake nyota, Said Dilunga dakika ya 58.
    Ushindi huo unaifanya Ruvu Shooting ifikishe pointi 23 na kupanda hadi nafasi ya 11 kutoka ya 16, wakati Ndanda FC inabaki nafasi ya 17 na pointi zake 19 za mechi 19 kwenye Ligi Kuu ya timu 20.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KMC YAIPIGA JKT UHURU, RUVU SHOOTING YAICHAPA NDANDA NANGWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top