• HABARI MPYA

  Saturday, December 18, 2021

  TANZANITE WAZISHINDA HILA ZA WARUNDI, WASONGA MBELE  PAMOJA na kucheza nane, timu ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite imelazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, Burundi leo katika mchezo wa marudiano Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia jioni ya leo Jijini Bujumbura.
  Tanzanite inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-3 baada ya kushinda 3-2 katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita Dar es Salaam na sasa itamenyana na Ethiopia katika Raundi ya Tatu.
  Kabla ya mechi wachezaji 11 wa Tanzanite waliambiwa wana maambukizi ya virusi vya Corona, hivyo kulazimika kucheza nane muda wote.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANITE WAZISHINDA HILA ZA WARUNDI, WASONGA MBELE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top