• HABARI MPYA

  Thursday, December 09, 2021

  AZAM FC YAONGEZA KOCHA MMAREKANI MSOMALI


  KLABU ya Azam FC imeingia mkataba wa miaka miwili na Kocha Abdihamid Moallin, kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa kituo cha kukuza vipaji (Azam FC Academy).
  Moallin ambaye ni Mmarekani mwenye asili ya Somalia, alisaini mkataba rasmi Jumamosi mbele ya Ofisa Mtendaji wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'.
  Aidha, Moallin aliyewahi kuifundisha Horseed ya Somalia, pia atakuwa akifanya uchambuzi wa mechi (analysis) za timu kubwa ya Azam FC.
  Kocha huyo amewahi kufanya kazi kwenye Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS), katika timu ya Columbus Crew (2014-2016), kama Kocha Msaidizi wa timu hiyo na timu za vijana chini ya miaka 18 na 23.
  Aidha amehudumu pia katika timu ya D.C United kama Kocha Msaidizi mwaka 2019.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAONGEZA KOCHA MMAREKANI MSOMALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top