• HABARI MPYA

  Thursday, December 23, 2021

  GEITA GOLD YAICHAPA TANZANIA PRISONS 1-0


  WENYEJI, Geita Gold FC wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita. 
  Tanzania Prisons watalala vichwa chini, kwani bao lenyewe mchezaji wao, Adili Buha alijifunga dakika ya 53 katika harakati za kuokoa. 
  Kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi 11 na kupanda hadi nafasi ya nne, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake nane katika nafasi ya 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YAICHAPA TANZANIA PRISONS 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top