• HABARI MPYA

  Saturday, December 18, 2021

  BEN POL, FRIDA AMANI WAPEWA TUZO YA MAZINGIRA


  WASANII Behman Paul ‘Ben Pol na mwanadada Frida Aman wametunukiwa tuzo maalumu baada ya kuonesha mchango wao mkubwa katika Shughuli za Uhifadhi wa Mazingira.
   Ben Pol na Frida wamepokea tuzo hizo kutoka Taasisi ya Lead Foundation kutokana na mchango wao katika shughuli za uhifadhi wa Mazingira. 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NGOs) katika shughuli za uhifadhi wa mazingira.
  Dkt. Jafo ameyasema hayo akifungua Kongamano la Kukomboa Ardhi iliyochakaa katika Nyanda kame za Tanzania sanjari na Maadhimisho ya miaka 10 ya Shirika la Lead Foundation.
  Amesema kuwa kongamano hilo linatoa taswira ya namna gani NGOs zinashiriki kikamilifu katika kusukuma mbele agenda ya mazingira nchini hivyo kuwajengea uelewa kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulinda na kuhifadhi mazingira.
  Kongamano hili limeandaliwa na Lead Foundation na limeshirikisha wadau mbalimbali wa mazingira ndani na nje ya nchi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEN POL, FRIDA AMANI WAPEWA TUZO YA MAZINGIRA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top