• HABARI MPYA

  Tuesday, December 07, 2021

  SIMBA WAANZIA LUSAKA MAZOEZI DHIDI YA YANGA


  WACHEZAJI wa Simba SC wakifanya mazoezi Jijini Lusaka nchini Zambia kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.


  Simba ipo Lusaka tangu Ijumaa ambako walikwenda kumenyana na wenyeji, Red Arrows katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, ambao walifungwa 2-1, lakini wamefuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 4-2 kufuatia kushinda 3-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA WAANZIA LUSAKA MAZOEZI DHIDI YA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top