• HABARI MPYA

  Sunday, December 26, 2021

  PRISONS YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 KAITABA


  TIMU ya Tanzania Prisons imezinduka kwa ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Bao pekee la Tanzania Prisons ambayo mechi mbili zilizopita ilifungwa 2-1 na Yanga mjini Sumbawanga na 1-0 na Geita Gold mjini Geita, bao lake pekee katika mchezo wa leo limefungwa na Marco Mhilu dakika ya 78 akimalizia pasi ya Jeremiah Juma.
  Kwa ushindi huo katika mechi ya 11, Tanzania Prisons inafikisha pointi 11 na kusogea nafasi ya 10, wakati Kagera Sugar iliyopoteza mechi ya pili mfululizo nyumbani leo kufuatia kufungwa 2-0 na Mbeya Kwanza Desemba 22, inabaki na pointi zake tisa katika nafasi ya 13 sasa kufuatia kucheza mechi 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PRISONS YAICHAPA KAGERA SUGAR 1-0 KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top