• HABARI MPYA

  Monday, December 20, 2021

  COASTAL UNION YAIPIGA BIASHARA 1-0 MUSOMA


  WENYEJI, Biashara United wamechapwa bao 1-0 na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.
  Bao pekee la Wagosi wa Kaya jioni ya leo limefungwa na Hija Ugando dakika ya 36 na kwa ushindi huo, Coastal inafikisha pointi 14 na kupanda hadi nafasi ya tano, wakati Biashara inabaki na pointi zake nane katika nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAIPIGA BIASHARA 1-0 MUSOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top