• HABARI MPYA

  Thursday, December 23, 2021

  KOMBA WA TANZANIA KUPEPERUSHA KIBENDERA AFCON


  REFA Mtanzania, Frank KOMBA ameingizwa kwenye orodha ya waamuzi 64 watakaochezesha Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika nchini Cameroon Januari mwakani.
  Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema amebahatika kuwa Mtanzania pekee kupata nafasi ya kwenda kufanya kazi AFCON ya mwakani akiingia kwenye orodha ya waamuzi 32 wa pembeni.
  Orodha ya CAF pia waamuzi wa kati 24 na wanane wa kutumia Usaidizi wa Picha za Video (VAR), wote wakitoka katika jumla ya nchi 37.
  Fainali hizo zinatarajiwa kuanza Jumapili ya Januari 9 mwaka 2022 kwa ufunguzi wa mchezo kati ya wenyeji, Cameroon dhidi ya Burkina Faso Uwanja wa Olembe Jijini Yaounde.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOMBA WA TANZANIA KUPEPERUSHA KIBENDERA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top