• HABARI MPYA

  Tuesday, December 28, 2021

  KMC CHUPUCHUPU KUPIGWA NA RUVU CHAMAZI, 1-1


  BAO la dakika ya mwisho la Charles Ilamfya limeinusuru KMC kupoteza mechi nyumbani baada ya kutoa sare ya 1-1 na Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Ilamfya alifunga bao hilo dakika ya pili na ya mwisho ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida za mchezo huo, kufuatia Ruvu Shooting kutangulia kwa bao la Ally Kombo dakika ya 22.
  Kwa matokeo hayo, KMC inafikisha pointi 11 katika nafasi ya 12 na Ruvu Shooting sasa ina pointi 10 katika nafasi ya 14 kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 11.
  Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC CHUPUCHUPU KUPIGWA NA RUVU CHAMAZI, 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top