• HABARI MPYA

  Friday, December 10, 2021

  IDDI NADO AFANYIWA MRI, KIGONYA MALARIA

  NYOTA tegemeo wa Azam FC, Idd Suleiman 'Nado' amefanyiwa kipimo cha MRI ili kujua ukubwa wa maumivu ya goti lake la kulia baada kuumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar mwezi uliopita.
  Katika mchezo huo uliofanyika Novemba 30 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC ilishinda 1-0, bao pekee la Mkongo Idris Mbombo.
  Taarifa zaidi juu ya winga huyo hatari zinatarajiwa kutolewa kuanzia leo, lakini kipa Mganda, Mathias Kigonya, amepewa mapumziko maalum kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Malaria.


  Winga mwingine, Ayoub Lyanga, ambaye alifanyiwa upasuaji kutokana na mipasuko mitatu kwenye mifupa ya juu ya mdomo (maxila bone) inayofahamika kitaalamu kama lefort 1, 11 na 111), pia kuvunjika meno, anaendelea na mapumziko hadi Desemba 31.
  Lyanga anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi ya viungo (gym) Januari 1 mwakani, kabla ya kurudi uwanjani rasmi kuanzia Januari 17, mwakani.
  Lyanga aliumia Novemba 2, mwaka huu hapo hapo Azam Complex kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold FC.
  Naye beki Lusajo Mwaikenda aliyeumia kwenye ajali ya barabarani, yupo tayari kuanza rasmi mazoezi na wenzake muda wowote.
  Lusajo amekuwa akifanya mazoezi mepesi ya peke yake, katika kipindi chote tangu apate ajali hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IDDI NADO AFANYIWA MRI, KIGONYA MALARIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top