• HABARI MPYA

  Monday, December 20, 2021

  MWITIKIO UCHANGIAJI UJENZI WA UWANJA SIMBA WARIDHISHA


  MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salum Abdallah 'Try Again" amesema zoezi la wanachama kuchangia fedha leo za ujenzi wa Uwanja wa klabu hiyo linaendelea vizuri.
  Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Abdallah amesema ndani ya muda mfupi tanhu kuzinduliwa kwa zoezi hilo Desemba 17, idadi kubwa ya wanachama imechangia fedha.
  Mpango huu ni wazo la Mwanahisa mkuu Simba, Mohamed 'Mo' Dewji ambaye ameahidi kutoa Sh. Bilioni 2 ili wanachama wajazie klabu hiyo ijenge Uwanja wake kuepuka adha inazokutana nao kutumia Uwanja usio wake.
  Kwa sasa Simba ina Uwanja wa mazoezi tu, Mo Simba Arena uliopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na mechi zake za mashindano inatumia Uwanja wa Benjamin Mkapa.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWITIKIO UCHANGIAJI UJENZI WA UWANJA SIMBA WARIDHISHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top