• HABARI MPYA

  Sunday, December 12, 2021

  MTIBWA SUGAR YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wamepata ushindi wa kwanza wa msimu baada ya kuichapa Biashara United 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Mabao ya Mtibwa Sugar leo yamefungwa na Nzigamasabo Steve kwa penalti dakika ya 13 na Said Ndemla dakika ya 73 na kwa ushindi huo, timu hiyo inayofundishwa na kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog inafikisha pointi tano katika mchezo wa nane na kusogea nafasi ya 15 ikiizidi tu wastani wa mabao Geita Gold inayohamia mkiani.
  Biashara United kwa upande wao wanabaki na pointi zao nane za mechi nane sasa katika nafasi ya 11 kwenye ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAPATA USHINDI WA KWANZA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top