• HABARI MPYA

  Friday, December 17, 2021

  NAMUNGO FC YAWACHAPA MBEYA KWANZA 1-0 SOKOINE


  TIMU ya Namungo FC imepata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Kwa ushindi huo uliotokana na bao la mshambuliaji Relliant Lusajo dakika ya tisa, Namungo FC inafikisha pointi 11 na kupanda hadi nafasi ya sita, wakati Mbeya Kwanza inabaki na pointi zake saba na kushukia nafasi ya 15 baada ya timu zote kucheza mechi tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAWACHAPA MBEYA KWANZA 1-0 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top