• HABARI MPYA

  Wednesday, December 22, 2021

  AZAM FC YAACHANA RASMI NI SURE BOY BAADA YA MIAKA 15


  KLABU ya Azam FC imeachana rasmi na kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ baada ya kuitumikia timu hiyo tangu mwaka 2007 inapanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
  Taarifa ya Azam FC jioni ya leo imesema; “Alasiri ya leo Desemba 22, (Sure Boy) amekuja Azam Complex kuchukua barua yake ya kuruhusiwa kuondoka Azam Football Club (Release Letter),”.
  “Amekabidhiwa barua hiyo na afisa mtendaji mkuu, Abdulkarim Amin Popat. Kwa barua hiyo, ni rasmi sasa kwamba Salum Abubakary siyo tena mchezaji wa Azam Football Club. Tunamtakia kila la kheri,”.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAACHANA RASMI NI SURE BOY BAADA YA MIAKA 15 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top