• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 06, 2021

  MBEYA CITY YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 SOKOINE


  WENYEJI, Mbeya City wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Mbeya City leo yamefungwa na Hussein Masalanga dakika ya 42 na Paul Nonga dakika ya 88 na kwa ushindi huo timu hiyo inafikisha pointi 14 na kupanda nafasi ya tatu, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake12 ikishukia nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top