• HABARI MPYA

  Tuesday, December 14, 2021

  SIMBA YAICHAPA JKT 1-0 AZAM FEDERATION CUP


  MABINGWA watetezi, Simba SC wamefanikiwa kwenda Raundi ya Nne ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee mshambuliaji Mtanzania mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kibu Dennis Prosper dakika ya 27.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAICHAPA JKT 1-0 AZAM FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top