• HABARI MPYA

  Friday, December 10, 2021

  TANZANITE YACHAPWA 1-0 NA MABINTI WA UGANDA

  TIMU ya taifa ya wasichana ya Uganda imewafunga wenzao wa Tanzania 'Tanzanite' 1-0 katika mchezo wa kirafiki jioni ya Alhamisi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Bao pekee la Uganda 'Created Cranes' limefungwa na Khadija Nandago dakika ya 18 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Janet Simba kufuatia mpira wa adhabu wa Samalie Nakacwa kutoka upande wa kulia baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Protasia Mbunda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANITE YACHAPWA 1-0 NA MABINTI WA UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top