• HABARI MPYA

  Friday, December 17, 2021

  DODOMA JIJI YALAZIMISHWA SARE NA POLISI JAMHURI


  WENYEJI, Dodoma Jiji FC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Wageni walitangulia kwa bao la kujifunga la Augustine Samson dakika ya 26, kabla ya Anuary Jabir kuisawazishia Dodoma Jiji dakika ya 62.
  Kwa sare hiyo, Dodoma Jiji inafikisha pointi 13 katika nafasi ya tano, ikizidiwa pointi mbili na Polisi Tanzania inayoshika nafasi ya tatu baada ya timu zote kucheza mechi tisa sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YALAZIMISHWA SARE NA POLISI JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top