• HABARI MPYA

  Friday, December 17, 2021

  GEITA GOLD YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-1

  TIMU ya Geita Gold imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
  Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Danny Lyanga dakika ya tatu na George Mpole dakika ya 90 na ushei, wakati la Ruvu Shooting alijifunga Nashon Naftali dakika ya 45.
  Kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi nane na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya 14, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake tisa katika nafasi ya 11 baada ya timu zote kucheza mechi tisa sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YAICHAPA RUVU SHOOTING 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top