• HABARI MPYA

    Thursday, December 16, 2021

    DUBE APIGA MBILI AZAM FC YAUA 4-0 CHAMAZI

    WENYEJI, Azam FC wamefanikiwa kwenda Raundi ya Nne Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Green Warriors usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
    Mabao ya Azam FC yamefungwa na washambuliaji Mkongo, Idris Mbombo dakika ya nne, Prince Dube Mpumelelo mawili dakika ya 65 na 86 na Mzimbabwe mwenzake, kiungo Never Tigere dakika ya 85.
    Ulikuwa mchezo wa kwanza Azam FC baada ya kumfukuza kocha Mzambia, George Lwandamina, ukimpa mwanzo mzuri kocha anayekaimu, Mmarekani mzaliwa wa Somalia, Abdihamid Moalin.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DUBE APIGA MBILI AZAM FC YAUA 4-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top