• HABARI MPYA

  Tuesday, December 28, 2021

  MTIBWA SUGAR YAILAZA COASTAL UNION 1-0 MKWAKWANI


  TIMU ya Mtibwa Sugar imepata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Bao pekee la Mtibwa Sugar katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo Salum Kihimbwa kwa penalti dakika ya 27.
  Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar imefikisha pointi 10 na kujiinua kutoka mkiani hadi nafasi ya 12, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 17 katika nafasi ya nne baada ya timu zote kucheza mechi 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAILAZA COASTAL UNION 1-0 MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top